Friday, September 6, 2013

Tafakuri kuhusu Ajira



Abert Sanga, Iringa — Mara kadhaa nimekuwa nikirudia kusema namna mifumo ya elimu zetu inavyoharibu wasomi wetu kuwa tegemezi. Licha ya ukweli kwamba ajira hakuna lakini wahitimu wengi wa vyuo bado wamekomaa na "KUSUBIRIA AJIRA". Licha ya ukweli kuwa mishahara wanayolipwa waajiriwa ni kiduchu kutimiza ndoto za maisha; lakini wasomi wetu bado wanaridhika kuvaa tai na kujifungia kwenye viyoyozi pasipo kufikiria namna ya kuongeza kipato. 

Wiki chache zilizopita niliandika status inayomuhusu kijana mmoja rafiki yangu aitwaye Meshack Maganga na namna alivyofanikiwa kiuchumi kwa kuanza na mtaji wa tsh. 25,000/=.
 

Wengi waliipenda lakini kuna kijana mmoja tu hadi sasa aitwaye Emmanuel Omary Mbedule ambaye alichukua
hatua baada ya kusoma status hiyo. KIjana huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo Kikuu cha Mkwawa; ambapo alinitafuta hadi kunipata na kuomba maelekezo kuhusu kilimo cha mbogamboga kilichomtoa Bw. Maganga. Nami kwa moyo wa furaha nikamkutanisha kijana huyu na Maganga. 

Leo ninavyoandika status hii tayari kijana huyu ameshapata shamba takribani robo tatu eka eneo la Kalenga-Iringa na anaendelea na shughuli za kulima mbogamboga.

Aidha, Meshack Maganga ana mashamba yake  ya miti ambayo baadhi anayauza kwa anae hitaji unaweza kuwasiliana nae kwa email yake
 meshackmaganga@gmail.com. 

Kwa mujibu wa Bw. Maganga ni kuwa kijana huyu amepanga kuingiza mtaji wa tsh. laki nne lakini kwa miezi mitatu hadi kuvuna mazao yake atapata fedha zisizopungua milioni tatu! IKumbukwe kuwa kijana huyu ni mwanachuo kama walivyo wanachuo wengine ambao mara zote hujifanya wako bize sana na tests, assignements, lectures na madikodiko mengine ya ki-rat race!

Hebu fikiria, ikiwa kijana kama huyu akawa anazalisha tsh. 3M kila
 semester; kwa miaka mitatu atakuwa na cash ya tsh 18Million. Patamu hapa! Unategemea huyu atahangaika kuwaza ajira? Sidhani! Ni nini kinafanya vijana wengine washindwe kuthubutu kujituma na kujaribu mambo licha ya kuwa wapo katika hali mbaya kiuchumi? NI nini kinafanya wengi wawe wazito kuchangamkia fursa kila zinapojitokeza? Shida ya wasomi wetu ndio hii; wana mbwembwe na maneno meeeeengiiii lakini hakuna chochote cha maana wanacho-display kwenye maisha yao.

Ukiwapa mifano na siri za wanaofanikiwa (km Wachaga), utasikia wanajifanya ma-
critical thinker wa kuwakosoa ilhali hawana mbele wala nyuma zaidi ya u-rat race tu. Ilete digrii yako, weka na masters, changanya na Phd zako; LAKINI kama huna mafanikio ya kujivunia kiuchumi: UTAKUWA KITUKO TU! 

No comments:

Post a Comment